- Get link
- X
- Other Apps
Viongozi wa Mataifa mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria sherehe za kumkabidhi madaraka rais mpya wa Jamhuri ya Malawi hii leo.
Mutharika kuapishwa kama rais mpya malawi |
Shughuli hiyo itafanyika kwenye uwanja wa Taifa wa Kamuzu uliopo jijini Blantyre ambapo Bw. Mutharika atapokea mamlaka ya juu ya nchi hiyo kutoka kwa Dr Joyce Hilda Banda ambaye ameongoza Malawi kwa miaka 2 iliyopita ikiwa ni baada ya kufariki kwa Rais Bingu wa Mutharika.
Jumamosi asubuhi Jaji mkuu Anastazia Msosa alimwapisha Mutharika kuwa Rais wa tano wa Malawi ikiwa ni saa 12 tu baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliokuwa umejaa malalamiko ya wizi wa kura na pingamizi mahakamani.
Akizungumza nyumbani kwake baada ya kula kiapo, Rais Mutharika amewaahidi wamalawi uhudumu bora na kumaliza kiu yao ya maendeleo, huku akiwataka wapinzani wake katika mbio za urais akiwemo Dr Joyce Banda waungane naye kuijenga Malawi.
Dr Banda pamoja na wagombea urais wengine 11 walioshindwa, wamempongeza Rais mpya na kuwataka wafuasi wao kukubali matokeo na kujipanga upya kwa uchaguzi ujao wa mwaka 2019
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment